Waamini Msikate Tamaa Changamoto Ni Sehemu Ya Maisha- Ask.Msonganzila

25/03/2024

Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila amewakumbusha wakristo nchini kuacha kukata tamaa hasa wanapokumbana na changamoto mbalimbali katika maisha, bali wamtazame Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yao.

Askofu Msonganzila ameyasema hayo wakati wa Misa Takatifu ya jumapili ya matawi aliyoiadhimisha Kanisa kuu la Maria Mtakatifu Mama wa Mungu Musoma, ambapo amesema kumekuwepo na tabia ya watu kutokukubali changamoto za maisha wanazokumbana nazo katika ndoa au utafutaji wa riziki badala yake wanaamua kuchukua maamuzi magumu hata ya kujitoa uhai.

Flowers in Chania

Tumtazame Yesu Kristo mateso aliyoyapitia ,lakini hakukata tamaa inakuwaje wewe unapitia changamoto kidogo tu unajitoa uhai.Tusimame imara katika imani na tuwe tayari kukabiliana nazo, na zinapokuelemea basi mpelekee Kristo maana alishatuahidi kuwa wote wenye mizigo waipeleke kwake naye atawapumzishaAmesema Askofu huyo.

Ameongeza kuwa katika maisha kuna watu ambao ni wa karibu sana lakini wamekuwa ndio chanzo cha maumivu ya watu wengine, hivyo hatuna budi kuwasamehe kwa kuwa hata Kristo amekuwa akitusamehe kila tunapofanya makosa .

Paroko wa Parokia hiyo Padri Medard Chegere amemshukuru Mhashamu Baba Askofu kwa kufika na kuongoza misa hiyo ya jumapili ya matawi.