Tuwasaidie Wahitaji - Wanafunzi wa shule ya St. John Bosco

24/02/2024

Wanafunzi wa shule ya St. John Bosco iliyopo Jimbo Katoliki la Musoma wamewaomba watu wote wenye nia njema na nafasi ya kuwasaidia wengine kuwakumbuka wahitaji,na kwa kufanya hivyo wataweza kujipatia baraka kutoka kwa Mungu.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada wa vitu mbalimbali Maria Bhoke amesema lengo la kufika katika Kituo cha Jipe Moyo na St. Justine ambavyo vinalea watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali ni kutaka kuwaonyesha upendo na kuwa tia moyo kwa changamoto za maisha wanazo pitia,lakini pia kuwakumbusha kuwa hawako peke yao bali jamii inayowazunguka bado inawapenda.

Flowers in Chania

Tumekuja hapa kuwaona wenzetu na kuwapatia kile tulichojaliwa na mwenyezi Mungu,ni kweli tunatofautiana hali ya maisha katika familia zetu ndio maana tumeona kwa kile tulichojaaliwa basi tuwapatie na wenzetu japo ni kidogo lakini basi kwa kuunganisha nguvu ya pamoja kama wanafunzi tumeweza kuleta kitu kinachoonekanaamesema Bhoke.

Akizungumza kwa niaba ya watoto walio pokea msaada huo Bahati ambaye ni mlemavu wa mikono na hana mkono hata mmoja anayetumia mguu kufua,kuandika na hata kula amewashukuru wanafunzi hao kwa kufika katika kituo hicho cha St. Justine na kwa kweli wameonyesha upendo wa hali ya juu sana.

Flowers in Chania

Msimamizi wa kituo cha Jipe moyo Sista Josephina Dismas amewapongeza walimu na walezi wa shule ya St. John Bosco kwa kuwafundisha wanafunzie namna bora ya kujali wahitaji na hivyo kutenga muda wa kwenda kukaa nao na kucheza nao sambamba na kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu kama vile kalamu,daftari,viatu,nguo na sabuni. Sista Josephina amesema kitendo walichokifanya walimu hakiwezi kuondoka kichwani kwa watoto hao na hivyo itakuwa moja ya somo ambalo wataliishi katika maisha yao yote.

Mkuu wa shule ya St. John Bosco Sista Maria Salome amesema kila mwaka huwa wanakuwa na siku ya Mtakatifu somo wao na hivyo huitumia siku hiyo kufanya matendo ya huruma na upendo kwa wahitaji kama somo wao alivyokuwa anafanya.